ATP inaweza kukusaidia kupata akili na nguvu ya kufanya jambo ambalo katika hali ya kawaida lisingewezekana. Wakati mwingine unaweza kufanya jambo hata wewe mwenyewe ukashangaa umelifanyaje. Unaweza kwa mfano kufukuzwa na mnyama mkali ukapenya mahali ambapo, katika hali ya kawaida usingepenya. Sasa usishangae tena. Kilichofanya upenye ni ATP.